Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HUDUMA ZA WAGONJWA DHARURA NA AJALI

Posted on: March 29th, 2024

Jengo la Idara ya Wagonjwa wa Dharura na Ajali

Idara ya Wagonjwa wa dharula na ajali

Idara hii ni moja kati ya Idara zilizokamilika na kujitosheleza kihuduma katika miaka ya hivi karibuni katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa. Mwaka huu 2019 kitengo cha Mapokezi (Casualty ) kilifanyiwa marekebisho makubwa yaliyopelekea kuzaliwa kwa vitengo viwili vya idara hii ambavyo ni Kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) na Kitengo cha wagonjwa wa dharura (EMD)

Muundo:

Kitengo cha Huduma kwa wagonjwa wa nje kinafanywa na:-

  1. Kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD)
  2. Kitengo cha wagonjwa wa dharura (EMD)
  3. Kitengo cha wagonjwa wa Bima

Ilipo Idara:

Idara inatazamana na geti kuu la kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, karibu na jengo la kitengo cha magonjwa ya akili (psychiatric unit), kitengo cha wagonjwa wa meno na Maabara kwa Upande wa kushoto.

Huduma tunazotoa:

Kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD)

  1. Huduma ya kuonwa na daktari
  2. Uchunguzi wa kitabibu
  3. Huduma za vipimo kushirikiana na vitengo vingine kama vile maabara
  4. Huduma za Elimu ya afya na Ushauri

Kitengo cha wagonjwa wa dharura (EMD)

  1. Kuona wagonjwa wote wa dharura na kuwaimarisha kabla ya kwenda wodini au chumba chaupasuaji, au wodi ya wagonjwa mahututi.
  2. Kufanya huduma za uchunguzi za dharura (P.O.C tests) kama vile (ECG, ABG, POC echo, FAST etc
  3. Kutoa huduma ya dharura kuokoa maisha ya wagonjwa (lifesaving interventions)
  4. Mafunzo ya utoaji huduma za dharura (Basic emergency care) kwa wafanyakazi wa idara, wafanyakazi kutoka hospitali zingine, wanafunzi wa ndani na nje ya nchi
  5. Huduma za dawa kwa wagonjwa wa dharura EMD

Huduma zitolewazo

  •  Kuona wagonjwa wote wa dharura na kuwaimarisha kabla ya kwenda wodini au chumba chaupasuaji, au wodi ya wagonjwa mahututi.
  • Kuona wagonjwa wa kawaida (Que patients)
  • Kufanya huduma za uchunguzi za dharura (P.O.C tests)
  • Kutoa huduma ya dharura kuokoa maisha ya wagonjwa (lifesaving interventions)

Mafunzo.

  • Idara inatoa mafunzo ya utoaji huduma za dharura (Basic emergency care) kwa wafanyakazi wa idara, wafanyakazi kutoka hospitali zingine, wanafunzi wa ndani na nje ya nchi


Picha ikionyesha baadhi ya matukio wakati wa Mafunzo ya kuhudumia mgonjwa wa dharura

Huduma zetu hutolewa na jopo la madaktari wenye weledi wakiwemo madaktari wazoefu ngazi ya digrii, Madaktari katika mafunzo ya Utarajali (Internship), na manesi wakiongozwa na daktari Bingwa.


T
Timu ya Madaktrai wa Idara ya wagonjwa wa Dharura na Ajali