WATARAJALI ST. JOSEPH WAENDESHA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU HOSPITALI YA BOMBO
Posted on: August 14th, 2025
Picha mbalimbali za matukio katika zoezi la uchangiaji damu lililoandaliwa na watarajali wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph (SJUIT) kutoka kada za Udaktari,Uuguzi na Famasi wanaoendelea na mafunzo kwa vitendo Hospitalini hapa. Zoezi hilo limefanyika mapema leo Agosti 14,2025 katika Jengo la Benki ya Damu lililopo Hospitali hapa ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa damu na kampeni zake za kuihamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari.
Mchango wako unaweza kuwa tegemeo kwa waathirika wa ajali, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watu wanaoendelea na matibabu na mengine mengi.
Kumbuka, kila unaposhiriki katika mazoezi mbalimbali ya kuchangia damu na huduma za uchangiaji damu, na kujitolea kwako kwa maandalizi rafiki na yanayofaa kwa kufuata miongozo na pia ni jambo la kupongezwa. Mchango wako ni nguzo muhimu inayodumisha jamii na inatoa zawadi ya maisha kwa wale wanaotegemea wema wa wafadhili kama wewe.
Changia Damu, Okoa Maisha.