Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HOSPITALI YAKABIDHIWA VITI TOKA TPPL

Posted on: December 19th, 2019

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, imekabidhiwa Viti vya kukalia wateja wakati wakisubiri huduma. Viti hivyo vimetolewa na Kampuni ya Tanga Pharmacetical and Plastic Limited (TPPL) na kukabidhiwa na Afisa Rasilimali watu wa kampuni hiyo Bi. Jenipher A. Mburuja. Wakati wa kukabidhi viti hivyo, Bi Jenipher Mburuja alisema kama kampuni wanajisikia furaha katika kupata nafasi ya kushiriki katika kuboresha Huduma zinazotolewa hospitalini hapo. Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Dr. Naima Zakaria ameshukuru kwa msaada huo na kuhakikisha kuwa viti hivo vitatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa ili kuboresha huduma katika hospitali yetu.Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Tanga Pharmacetical and Plastic Limited Bi. Jenipher A. Mburuja (Katikati) akiwa na Katibu wa Afya Mkoa wa Tanga Bw. Amiri Gogora (Kulia) Pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Tanga Dr. Naima Zakaria mara baada ya Kukabidhi viti vya kukalia wateja wakati wakisubiri kupata huduma.