ELIMU KWA JAMII JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA AFYA MAONI.
Posted on: June 4th, 2025ELIMU KWA JAMII JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA AFYA MAONI.
Mapema leo Juni 4,2025 Mhamasishaji wa mfumo wa Afya Maoni Ndg. Faraja Kampambe ametoa Elimu kwa jamii kuhusiana na Mfumo huo wa kukusanya maoni kidigitali kwa kutumia simu ya mkononi kupitia kipindi cha Amka na Maarifa kinachoruka kila siku za wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kupitia Redio Maarifa FM iliyopo hapa jijini Tanga.
Katika kipindi hicho Bw. Kampambe amewaasa wananchi wa Mkoa wa Tanga wanaokuja kupatiwa huduma za afya Hospitalini hapa pamoja na Vituo vya Afya kuutumia mfumo huo kuwasilisha kero,malalamiko, ushauri au pongezi kupitia njia rahisi tu ya simu zao za mkononi ambapo huduma hizo ni bure.
"Katika kuhakikisha Serikali inaimarisha kasi na ufanisi katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake Wizara ya Afya imeanzisha mfumo maalum wa kutoa maoni ambao unazingatia usiri na haki ya mtoa maoni ambao kwa sasa zoezi la utoaji maoni hukamilika ndani ya saa 4 tu ukiwa na simu yako ya mkononi".
Amesema "Njia hii rahisi kwani unaweza kutuma ujumbe wako mfupi wa neno MAONI kwenda nambari 15077 kisha fuata maelekezo ya Mhudumu wetu wa Huduma kwa wateja hadi pale utakapokamilisha huduma yako na namba ya kituo kwa Hospitali ya Bombo ni 10040500 na huduma hii inapatikana bure bila makato yoyote kwa watumiaji wa mitandao ya Yas, Airtel na Vodacom".



