Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

COASTAL UNION, AFRICAN SPORTS WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO

Posted on: February 4th, 2024

MASHABIKI wa timu ya African Sports na Coastal Union leo wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa ajili ya Kitengo cha Damu salama kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo .

Uchangiaji huo umefanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo mashabiki hao walijitokeza kwa wingi kuchangia damu ikiwa ni kuelekea mechi ya watani wa Jadi kwenye uwanja huo ambao ni deby ya watani wa jadi. 

Akizungumzia zoezi hilo Afisa Habari wa timu ya Coastal Union Miraji Wandi alisema kwamba chama cha Mapinduzi (CCM) nndio kimewezesha matukio hayo katika kusheherekea miaka 47 ya kuzaliwa kwanza 

Alisema kwamba linapokuja suala la kuchangia damu salama alijitokeza mdau who’s Hussein Foundation, Dewji Foundation ambaye amechangia kwa kutoa motisha jezi kwa mashabiki wanaojitikjeza kuchangia.

 “Motisha hiyo inawapa hari mchangiaji nguvu ya ziada vipo vitu mwana damu anaweza kuchangia lakini ni jambo la kiungwana na kupelekea mashabiki wa kujitokeza kwa wingi kubwa tunataka kufikia malengo ya upatikanaji wa damu iliyokuwa inahitajika”Alisema 

Hata hivyo aliweapongeza watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga kitengo cha Damu Salama kwa kufanya kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi hususani waliojitokeza kutoa damu.

“Hivyo niwapongeza watumishi kwa uzalendo wao na waledi mkubwa Katika kuwahudumia wachangiaji ambao wamekuja kuchangia damu katika viwanja hivi vya Mkwakwani “Alisema