Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

HUDUMA YA GARI LA DHARULA

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, inapenda kuwataarifu wananchi wa mkoa wa Tanga na watanzania kwa ujumla kuwa, imeanzisha huduma ya Gari la dharula kwa wananchi watakaohitaji huduma hiyo ndani ya  Tanga Jiji. Huduma hii ni katika kuboresha huduma zetu ambazo zitasaidia wananchi wenye wagonjwa mahututi kupiga simu na kufikiwa na huduma hiyo ambapo mgonjwa ataanza kupatiwa huduma ya Kwanza kabla ya kufikishwa Hospitalini. Jambo hili litasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na ucheleweshaji wa wagonjwa kufika hospitalini bila kupata Huduma ya Kwanza


- 30 January 2020