Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

TOUCH HEALTH WATEMBELEA BOMBO-TANGA KUBORESHA AFYA KUPITIA TEKNOLOJIA.

Posted on: August 24th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo leo, Agosti 24, 2026, imepokea ugeni kutoka Taasisi ya Touch Health, inayoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha na kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia.

Ugeni huo umekutana na Uongozi pamoja na Timu ya Ufundi ya Hospitali ya Bombo, ambapo wataalam hao wamepata fursa ya kupitia maeneo mbalimbali ya kiufundi yanayohusiana na mifumo na miundombinu ya hospitali, kwa lengo la kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.

Mshauri wa Ufundi kutoka Taasisi ya Touch Health, Bw. Masanja Damian, amesema taasisi hiyo inaendelea kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa Timu ya Ufundi ya Hospitali ya Bombo ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuhakikisha teknolojia na mifumo ya hospitali inafanya kazi kwa kiwango kinachokidhi mahitaji ya wananchi.

Amesema ushirikiano huo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Tanga wanapata huduma bora, salama na zenye ufanisi kupitia matumizi sahihi ya teknolojia katika sekta ya afya.