Wasiliana nasi | FAQ | Mails | Malalamiko |

Tanga Regional Referral Hospital
(Bombo Hospital)

"NIMEZINDUKA NIKIWA BOMBO, NAWASHUKURU WATUMISHI NA UONGOZI WA BOMBO”.

Posted on: August 24th, 2026

Paulina Mgurwasasa, mkazi wa Tanga Mjini, ametoa shukrani zake kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo baada ya kupata matibabu na kupona hali iliyokuwa ikihatarisha maisha yake.

Alifikishwa katika Hospitali ya Bombo akiwa amepoteza fahamu lakini baada ya kupokelewa, wataalam walichukua hatua za haraka za kitabibu na kuanza kumhudumia kwa karibu katika Wodi Binafsi.

Jitihada, ufuatiliaji na huduma za wataalam zilisaidia kurejesha hali yake jambo lililomfanya kutoa shukrani kwa watumishi na uongozi wa hospitali kwa namna walivyomhudumia.

Tazama video hii kwa undani zaidi https://youtu.be/3FEuo3wdt3w